Maji ni muhimu kiuchumi, kijamii na
kimazingira.
Matumizi ya maji yanapozidi uwezo wa vyanzo husababisha upungufu na kupeleka ukosefu wa maji Kimsingi usimamizi na
ugawaji wa maji unahitajika. Tunatambua kuwa Maji yote ni mali ya Taifa na
yanasimamiwa chini ya sheria ya usimamizi wa rasilimali za maji Na. 11 ya mwaka
2009.Lengo la sheria hii ni
kuratibu na kusimamia matumizi ya maji na kuzuia uchafuzi wa vyanzo. Kila mtu
aliyechukua au anayetaka kuchukua maji kwa matumizi yoyote anapaswa kuwa na hati ya kumiliki maji.
LNBWB ni
nini ?
LNBWB ni
ofisi inayosimamia na kuratibu
matumizi ya bonde la Ziwa Nyasa.
Ni yapi majukumu ya Ofisi ya
Bonde la Ziwa Nyasa?
Kusimamia na
kuratibu matumizi bora ya maji. Kudhibiti na
kuchukua hatua dhidi ya wachafuzi
wa
maji na vyanzo vyake. kutoa vibali vya kutumia maji
Ni
changamoto gani zipo katika usimamizi wa
rasilimali za maji?
Watu wengi wamekuwa
wanatumia maji bila vibali. Matumizi
makubwa ya maji
zaidi ya kiwango kinachohitajika. Watu wengi
wana imani kuwa maji ni zawadi
toka kwa Mungu na
haipaswi kulipiwa kama rasilimali nyingine. Uharibifu
mkubwa
katika vyanzo vya maji kutokana na ongezeko la watu. Upungufu wa maji katika
vyanzo vingi
Bodi
ya Maji ya Bonde imechukua hatua gani
katika kusimamia vyanzo vya maji na kuwa
na
uhakika wa maji
Bodi
ya Maji ya Bonde la Ziwa Nyasa katika kulinda na kutunza
vyanzo vya
maji,imeweza kuainisha vyanzo vya maji na
kushirikisha jamii husika katika
UNAFAIDIKA NA NINI HUDUMA
ZITOLEWAZO.
Huduma zitolewazo........................
- Kupata kibali kinachokulinda kisheria
- Visima vingi hukauka mara kwa mara, kutokana na kutofuata taratibu za uchimbaji na kutokuwa na utafiti wa kina. Sajili kisima chako katika Ofisi za Bonde ili kisima chako kiwe na uhakika wa maji.
- Ofisi ya Bonde ndio inayoweza kukupa utatuzi wa migogoro ya matumizi ya Maji.
- Kupitia jumuiya za watumia maji,vidakio,na bodi ya bonde znakushirikisha katika katika suala zima l;a usimamizi wa rasili mali maji
BONDE LA ZIWA NYASA
Hili ni eneo lote ambalo mwelekeo wa maji yake hatimaye huingia kaitka Ziwa Nyasa .
Eneo hili linajumuisha mikoa ya Mbeya,Njombe na Ruvuma.
Wateja wengi wamenufaika na huduma zetu 485 Makampuni mashirika na Tasisi za binafsi wanavibali vya maji.
Kwa
maelezo zaidi fika Ofisi ya Bonde ya Ziwa Nyasa Tukuyu
Wizara ya Maji
OfisiyaBonde la ZiwaNyasa
P.O. Box240 TUKUYU
+255 2552250
nyasabasin@yahoo.com
www.lakenyasabasin.com
Ofisi Ndogo Songea
P.O. Box 42, SONGEA
+25525260166
nyasabasinsuboffice@yahoo.com
www.lakenyasabasin.com
No comments:
Post a Comment