Wednesday, 12 August 2015

WIZARA YA MAJI NA RASILIMALI YA MAJI WAKIELIMISHA WANANCHI SIKU YA NANENANE KILIMO,VYOMBO VYA HABARI WAKIUNGANA NA RADIO GENERATION FM


Wizara ya Maji wakiwasilisha taarifa kupitia vyombo ya habari kuhusu rasilimali za maji na vyanzo vya maji kupitia maonyesho ya nanenane,Hivyo basi wizara ya maji inawakumbusha wananchi kupata vibari vya maji kupitia Ofisi za bonde la Ziwa Nyasa Tukuyu,Ofisi ya Ziwa Rukwa Mbeya na Ofisi ya Mto Rufiji Iringa 


Generation FM wakitembelea banda la Wizara ya Maji katika maonyesho ya sikukuu ya nanenane Jijini Mbeya 

Vijana wengi wakipata mafunzo na maelezo kuhusu mfumo mzima wa maji na vyanzo vya maji kupitia Tekonologia mbalimbali na jinsi ya kutunza Rasilimali ya maji na vyanzo vyake,hapa tunaona vijana wakielimishwa jinsi ya kutumia boti ukiwa ndani ya maji.


    Hivi hapa ni vifaa vinavyo tumika kupima  kiasi cha maji na  hawa ni vijana wametembelea wizara ya maji na Vyanzo vya maji na kuona matumizi ya maji na Rasilimali ya maji.

                                            
Hapa kuna vifaa vingi vinavyo tumika kupima maji chini ya Aridhi,kunawatalaam wanao pima visima na kutoa kibari cha uchimbaji visima kwa manufaa ya rasilimali ya maji kupitia mabonde ya maji na wizara ya maji kwa kiwango kinacho hitajika       


Vyote hivi vilitumika katika maonyesho ya Nanenane



Kila kifaa na kazi yake kila mtu alipenda kujua jinsi gani atatunza vyanzo vya maji





Monday, 10 August 2015

BONDE LA ZIWA RUKWA



Hili ni eneo lote ambalo mwelekeo wa maji yake hatimaye

huingia katika Ziwa Rukwa. Eneo hili linajumuisha mikoa ya Mbeya, Rukwa, Katavi na sehemu ndogo ya mkoa wa Tabora

Wateja wengi tayari wanafaidika na huduma zetu

1050
Makampuni, mashirika na taasisi za watu binafsiwanavibali vya matumizi ya maji


Usimamizi shirikishi wa rasilimali maji kupitia jumuiya za watumia maji

Kwa maelezo zaidi fika Ofisi ya Maji Bonde la Ziwa Rukwa - Mbeya

Ofisi ya Bonde la Ziwa Rukwa
P.O. Box 762, MBEYA
+255 2500028
rukwabasin@yahoo.com
www.lakerukwabasin.co.tz

 Ofisi Ndogo Sumbawanga
P.O. Box 192, SUMBAWANGA
+255252802034
rukwabasinsuboffice@yahoo.com
www.lakerukwabasin.com


UTANGULIZI WA RASILIMALI YA MAJI BONDE LA ZIWA NYASA TUKUYU



Maji ni muhimu kiuchumi, kijamii na

kimazingira.
Matumizi ya maji yanapozidi uwezo wa vyanzo husababisha upungufu na kupeleka ukosefu wa maji Kimsingi usimamizi na ugawaji wa maji unahitajika. Tunatambua kuwa Maji yote ni mali ya Taifa na yanasimamiwa chini ya sheria ya usimamizi wa rasilimali za maji Na. 11 ya mwaka 2009.Lengo la sheria hii ni kuratibu na kusimamia matumizi ya maji na kuzuia uchafuzi wa vyanzo. Kila mtu aliyechukua au anayetaka kuchukua maji kwa matumizi yoyote anapaswa kuwa na hati ya kumiliki maji.
 LNBWB ni nini ?

LNBWB ni ofisi inayosimamia na kuratibu 

matumizi ya bonde la Ziwa Nyasa.

Ni yapi majukumu ya Ofisi ya Bonde la Ziwa Nyasa? 

 Kusimamia na kuratibu matumizi bora ya maji. Kudhibiti na 

kuchukua hatua dhidi ya wachafuzi wa 

maji na vyanzo vyake. kutoa vibali vya kutumia maji

Ni changamoto gani zipo katika usimamizi wa

          rasilimali za maji?

 Watu wengi wamekuwa wanatumia maji bila vibali.  Matumizi

makubwa ya maji zaidi ya kiwango kinachohitajika. Watu wengi 

wana imani kuwa maji ni zawadi toka kwa Mungu na 

haipaswi kulipiwa kama rasilimali nyingine. Uharibifu 
mkubwa 

katika vyanzo vya maji kutokana na ongezeko la watu. Upungufu wa maji katika vyanzo vingi

 Bodi ya Maji ya Bonde imechukua hatua gani 

katika kusimamia vyanzo vya maji na kuwa na

uhakika wa maji

    Bodi ya Maji ya Bonde la Ziwa Nyasa katika kulinda na kutunza

vyanzo vya maji,imeweza kuainisha vyanzo vya maji na 
kushirikisha jamii husika katika 



UNAFAIDIKA NA NINI HUDUMA 

ZITOLEWAZO.



                 Huduma zitolewazo........................

  1. Kupata kibali kinachokulinda kisheria 
  2.   Visima vingi hukauka mara kwa mara, kutokana na kutofuata taratibu za uchimbaji na kutokuwa na utafiti wa kina. Sajili kisima chako katika Ofisi za Bonde ili kisima chako kiwe na uhakika wa maji.
  3. Ofisi ya Bonde ndio inayoweza kukupa utatuzi wa migogoro ya matumizi ya Maji.
  4. Kupitia jumuiya za watumia maji,vidakio,na bodi ya bonde znakushirikisha katika  katika suala zima l;a usimamizi wa rasili mali maji

                       BONDE LA ZIWA NYASA
Hili ni eneo lote ambalo mwelekeo wa maji yake hatimaye huingia kaitka Ziwa Nyasa .
Eneo hili linajumuisha mikoa ya Mbeya,Njombe na Ruvuma.

Wateja wengi wamenufaika na huduma zetu 485 Makampuni mashirika na Tasisi za binafsi wanavibali vya maji.

Kwa maelezo zaidi fika Ofisi ya Bonde ya Ziwa Nyasa Tukuyu
 Wizara ya Maji
OfisiyaBonde la ZiwaNyasa
P.O. Box240 TUKUYU
+255 2552250
nyasabasin@yahoo.com
www.lakenyasabasin.com

Ofisi Ndogo Songea
P.O. Box 42, SONGEA
+25525260166
nyasabasinsuboffice@yahoo.com
www.lakenyasabasin.com

WIZARA YA MAJI, RASIMALI ZA MAJI NA BODI ZA MABONDE

Bodi za Maji za Mabonde

Bonde ni nini?

Bonde la Ziwa Rukwa
Hili ni eneo lote ambalo mwelekeo wa maji yake hatimaye huingia katika Ziwa Rukwa. Eneo hili lina jumuisha mikoa ya Mbeya, Rukwa,Katavi na sehemu ndogo ya mkoa wa Tabora na Singida

Bonde la Ziwa Nyasa

Hili ni eneo lote ambalo mwelekeo wa maji yake hatimaye huingia katika Ziwa Nyasa.

Eneo hili linajumuisha mikoa ya Mbeya,
Njombe na Ruvuma.

Bonde la Mto Rufiji

Hili eneo lote ambalo mwelekeo wa
yake hatimaye huingia katika Mto Rufiji.
Eneo hili linajumuisha mikoa ya Iringa,Morogoro,Dodoma na sehemu ndogo ya mkoa wa Mbeya,Pwani,Ruvuma,Lindi na singida
Bodi hizi zinasimamia na kuratibu matumizi ya maji katika mabonde.











 Bodi ya Bonde la Ziwa Rukwa
P.O. Box 762, MBEYA
+255 2500028
rukwabasin@yahoo.com
www.lakerukwabasin.co.tz


 










 BodiyaBonde la Mto Rufiji  /    Bodi ya Bonde la Ziwa Nyasa 
P.O. Box 1798, IRINGA      /    P.O. Box 240, TUKUYU
+255 (26) 2720951-4          /    0754 769622 / 0753398141
info@rufijibasin.com           /     nyasabasin@yahoo.com
www.rufijibasin.com           /      www.lakenyasabasin.com

                                                                
HIZI NI OFISI  ZA MAJI BONDE LA ZIWA RUKWA,OFISI YA MAJI BONDE LA ZIWA NYASA TUKUYU NA OFISI YA MAJI BONDE LA MTO RUFIJI IRINGA.


KUSAJILI VISIMA

Kibali kitakulinda upate kuwa na uhakika wa  maji


Wizara ya Maji
Bodi ya Maji ya Bonde la Ziwa Rukwa
Bodi ya Maji ya Bonde  la Ziwa Nyasa
Bodi ya Maji ya Bonde la Mto Rufiji